Manchester United wameweka vipaumbele vyao vya uhamisho chini ya Sir Jim Ratcliffe na wanataka kusajili fowadi wa daraja la juu ambaye yuko katika kiwango sawa na Harry Kane.
Ratcliffe anatarajia dili lake la pauni bilioni moja la kununua asilimia 25 ya hisa za United kupitishwa mapema mwezi ujao na tayari anaendelea na mipango ya kufufua klabu hiyo.
Mshambuliaji mpya wa kati wa kuongeza mashambulizi ya United ametambuliwa kama kipaumbele, huku namba 8, beki wa kati na beki wa kulia pia akilengwa.
Mshambulizi yeyote mpya anatarajiwa kucheza pamoja na Rasmus Hojlund aliyesajiliwa kwa pauni milioni 72, ambaye alifunga bao lake la pili la Ligi Kuu ya England katika sare ya 2-2 na Tottenham jana.
Winga wa Crystal Palace Michael Olise ametambuliwa na United kama shabaha kuu ya uhamisho kabla ya marekebisho yaliyopangwa ya kikosi chao mwishoni mwa msimu huu.