Mtendaji mkuu wa Premier League Richard Masters anasema tarehe imepangwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa Manchester City kuhusu madai 115 ya ukiukwaji wa kanuni za fedha za ligi, lakini hatafichua lini.
Kwa mujibu wa Premier League, Man City, ambao walishtakiwa Februari 2023, wanadaiwa kuvunja kanuni kwa misimu tisa kati ya 2009 na 2018, ambapo walishinda taji la ligi mara tatu.
Everton na Nottingham Forest zilishtakiwa kwa kukiuka Kanuni za Faida na Uendelevu za Ligi Kuu mapema wiki hii – na Everton walikatwa pointi 10 mwezi Novemba kwa kosa lilo hilo.
“Ikiwa klabu yoyote, iwe ni mabingwa wa sasa au vinginevyo, ingepatikana katika ukiukaji wa sheria za matumizi ya mwaka ’23, itakuwa katika nafasi sawa na Everton au Nottingham Forest.
“Kuna tarehe imepangwa kwa ajili ya kesi hiyo. Kwa bahati mbaya, siwezi kuwaambia ni lini lakini hilo linaendelea.
Siwezi kutoa maelezo yoyote kuhusu Man City zaidi ya kusema tarehe imepangwa, siwezi kukuambia. tarehe hiyo ni lini.