Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya ,Renson Ingonga ameidhinisha mashtaka 10 dhidi ya mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie , wa kanisa la Good news Internatioanal,anayetuhumiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 430 eneo la Shakahola ,pwani ya nchi hiyo
Kiongozi wa mashtaka amesema baada ya kutathmini faili ya uchunguzi kutoka idara ya upelelezi ,kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki mchungaji Mackenzie na washirika wake 95 wanaohusishwa na vifo vya washirika wa kanisa hilo la kufunga hadi kufa.
Baadhi ya mashtaka dhidi ya Mackenzie ni mauaji na ugaidi mashtaka mengine yakiwa ni kuua bila kusudia na kusababisha majeraha ya mwili.
Kwa mujibu wa sheria ya Kenya ya kuzuia ugaidi na uhalifu wa kupangwa,watuhumiwa hao watashtakiwa kwa kuhusika kwenye uhalifu wa kupangwa na mafunzo yenye itikadi kali.