Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuanzisha operesheni ya pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Jumuiya ya Maendelezo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC dhidi ya waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.
Maafisa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congona wale wa kikosi cha mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, wamefanya mkutano wa tahmini ya hali ya kiusalama jimboni Kivu ya Kaskazini.
Kufuatia mkutano huo, Luteni Jenerali Fall Sikabwe, Kaimu Mkuu wa jeshi la Kongo DR amesema kuwa, jeshi la FARDC na kikosi cha SADC maarufu SAMIDRC wataanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa M23.
Kwa upande wake, naibu kamanda wa kikosi cha SADC nchini Kongo , Jenerali Julius Gambos kutoka Tanzania amesema lengo la kikosi hicho ni kuunga mkono jeshi la Kongo kuyasaka makundi ya waasi huko kwenye majimbo ya mashariki.
Serikali ya Jamhurii ya Kidemokrasia ya Congo, ilialika kikosi hicho cha SADC baada ya kusema kuwa haijaridhika na wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao walitakiwa kupambana na waasi wa M23.