Mara ya mwisho kwa fowadi wa Brentford, Ivan Toney kucheza mechi ya ushindani ilikuwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Liverpool Uwanja wa Anfield Mei mwaka jana.
Lakini kusimamishwa kwake kwa miezi minane, kwa kukiuka sheria za kamari, muda wake unaisha rasmi leo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatazamiwa kurejea katika mechi yake aliyoitarajia dhidi ya Nottingham Forest wikendi hii.
Alienda kwenye mtandao wa kijamii wa X Jumatano asubuhi kusherehekea kile kinachoitwa ‘uhuru’ wake.