Pakistan imeonya kuhusu “matokeo makubwa” baada ya Iran kufanya shambulio la kombora katika mkoa wa Balochistan kusini magharibi.
Nchi hizo mbili, zinazoshiriki mpaka wa takriban maili 559 kusini magharibi mwa Pakistan na kusini mashariki mwa Iran, zina uhusiano mgumu.
Wameshiriki maswala ya usalama, haswa kupambana na itikadi kali na ugaidi, na wamekuza ushirikiano katika maeneo kadhaa.
Katika siku za hivi karibuni, mwingiliano kati ya maafisa wa Pakistan na Iran umeongezeka.
Pakistan imekuwa ikikabiliwa na ghasia za miongo kadhaa za waasi wa Baloch wanaodai kujitenga na imeilaumu Iran siku za nyuma kwa mashambulizi ya wanamgambo yanayolenga vikosi vyake vya usalama.