Paris Saint-Germain wanatarajiwa kuongeza pauni milioni 200 katika bajeti ya klabu hiyo iwapo Kylian Mbappe ataondoka msimu huu wa joto.
PSG wanatatizika kumshawishi Mbappe, 25, kusaini mkataba mpya.
Mkataba uliopo wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa unaisha mwezi Juni na Real Madrid wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania saini yake.
Vilabu vya Uingereza, ikiwa ni pamoja na Liverpool, vitajaribu kumnasa kwenye Ligi ya Premia.
PSG wangependa kuendelea kumshikilia Mbappe, lakini wanaangalia vyema hali yake.
Wakuu wa PSG wanajaribu kuunda kikosi cha vijana – bila majina ya nyota – chini ya bosi Luis Enrique, baada ya kuwaondoa Messi na Neymar msimu uliopita wa joto, na kumwachilia Mbappe, inaeleweka, kungeongeza idadi ya pauni milioni 200 katika bajeti yao. .