Mashabiki wamekuwa wakizungumza mengi, huku wengine wakionyesha kusikitishwa na chapisho la hivi karibuni la nyota wa muziki wa Nigeria, Omah Lay.
Katika chapisho kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii (X) mnamo Jumanne, Januari 16, 2024, mwimbaji huyo wa ‘holly Ghost’ alifunguka kuhusu hali yake ya sasa ya kihisia na kusema kwamba hajisikii tena chochote kuhusu mapenzi.
Chapisho lake linasema, “Sijisikii chochote tena.”
Chapisho hili limezua wasiwasi miongoni mwa wafuasi wake, na kuzua maswali kuhusu hali yake ya kiafya huku wengine wakishuku kuwa mwimbaji huyo anakaribia kuachia wimbo mpya.
Wengi walimtia moyo kutumia hisia zake za sasa na kuunda ngoma kali studio kwaajili ya mashabiki wake.