Jordan Henderson atasafiri kwenda Amsterdam leo kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu ya Ajax baada ya kuafikiana kuhusu mkataba wa miaka miwili na nusu.
Sky Sports News iliripoti Jumatano kwamba wajumbe kutoka kwa klabu hiyo ya Uholanzi walikuwa wakisafiri kwa ndege kwenda Manchester kukamilisha masharti ya kandarasi ya Henderson, huku mikutano ikiendelea hadi usiku wa manane.
Ajax watamenyana na RKC Waalwijk katika Eredivisie Jumapili, na wako nyuma kwa pointi 23 dhidi ya viongozi wa ligi PSV.
Henderson hatastahili kucheza wikendi hii kwa sababu visa yake bado haijatolewa.