Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez, ambaye amekabiliwa na presha, alisema Jumatano kwamba atajiuzulu ikiwa kikosi chake hakitamwamini tena kufuatia kipigo kizito cha fainali ya Kombe la Super Cup ya Uhispania dhidi ya Real Madrid wikendi iliyopita.

Barcelona ilicharazwa 4-1 na Madrid siku ya Jumapili na kukaa pointi nane nyuma ya kiongozi Girona kwenye jedwali la La Liga. Katika safu ya ulinzi Wakatalunya hao wamejitahidi mwaka huu jambo ambalo ni tofauti kabisa na mafanikio ya msimu uliopita wa Liga.
Wameruhusu mabao 22 katika nusu ya msimu wa ligi baada ya kusafirisha 20 pekee katika kipindi chote cha kampeni za 2022-23.
“Siku ambayo wachezaji wangu hawatanifuata tena, nitafunga virago na kuondoka,” Xavi aliwaambia wanahabari.
“Kama singeshinda La Liga mwaka jana nisingekuwa hapa. Mtu akiniambia kuna tatizo, nitaondoka. Naipenda klabu hii. Niko hapa kuleta kitu kwake. Nisipofanya hivyo, nitarudi nyumbani,” nahodha huyo wa zamani wa Barca aliongeza.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43 alirejea kwa mabingwa hao wa Uhispania mnamo 2021 baada ya kudumu kama bosi wa Al Sadd.
Siku ya Alhamisi, Barcelona itamenyana na Unionistas wa daraja la tatu katika hatua ya 16 bora ya Copa del Rey kabla ya kucheza na Napoli katika mkondo wa kwanza wa hatua hiyo hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa mnamo Februari.