Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye,ameitka Bodi ya Tume ya ulinzi wa Taarifa binafsi kusimamia majukumu ya Tume hiyo, kwa kuzingatia sheria katika kuhakikisha inalinda ,haki na utu wa watu wa taarifa ili kujenga imani kwa watu wote hasa wanaotoka nje ili waone Tanzania ni sehemu salama.
Waziri Nnauye ametoa rai hiyo leo Januari 19,2024 jijini Dodoma na mara baada ya kuzindua Bodi hiyo ambapo ameitaka Bodi hiyo kuanza kutoa elimu kwa umma kuhusu ulinzi wa Taarifa binafsi kupitia makongamano mbalimbali ili wawe na uelewa.
Waziri Nnauye mesema tume hiyo mpya inajukumu la kulinda heshima, haki na utu kwa kuhakikisha taarifa za watanzania na hata wageni taarifa zao kuwa sehemu salama na zinatumika kwa kujali haki heshima na utu ili watu waone Tanzania ni taifa salama kwa huduma za kidigitali
“Wito wangu kwenu ni kuilinda imani ya Rais wetu kwani mchakato ulikuwa mkubwa kuwapata nyinyi na kuipata tume hii na ukweli kutoka moyoni ninatamani kuja kusikia tume hii ya taarifa binafsi nchini ni Bora kuliko tume nyingine duniani, ” Amesema Mhe. Nnauye
Aidha amesisitiza kuwa matumaini ya taifa ni kuona faragha zao zinalindwa nchini kwani kuanzia sasa taarifa za watu zinakusanywa ,zinachakatwa na kutuma sehemu sahihi ambapo misingi mikuu inazingatiwa ya kikanda na kimataifa .