WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hali uzalishaji wa sukari katika viwanda saba nchini imeshuka hadi kufikia tani 1,000 kwa siku kutokana na mvua za El-nino zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.
Amesema mvua hizo zimeathiri hali ya uvunaji wa miwa mashambani na kupunguza kiwango cha sukari katika miwa kwa zaidi ya asilimia 25.
Akitoa kauli ya serikali leo Jumamosi kuhusu hali ya sukari nchini, Bashe amesema katika kukabiliana na upungufu wa sukari ambao sasa umefikia tani 30,000, serikali imetoa kibali kwa wenye viwanda kuagiza sukari tani 100,000 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini tarehe 23 – 24 Januari mwaka huu.
Amesema mahitaji ya sukari kwa siku nchini ni tani 1,500 na kutokana na hali hiyo bei ya sukari imepanda kutoka 2,700, 3000 hadi kufikia 4000.