Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda asimamisha msafara wake na kumsikiliza Mwanamaa aliyekuwa amesimama pembezoni mwa barabara aliyenyoosha mkono ishara ya kuomba nafasi walau ya kumuona.
Mwenezi Makonda amesimamisha msafara huo leo tarehe 20 Januari, 2024 akiwa njiani kutokea Wilayani Handeni kuelekea Wilayani Pangani.
Mara baada ya kusimama, Alimsikiliza Mama huyo ambaye alijitambulisha na kujieleza kwake kuwa ni mjasiriamali na kutoa shukrani zake kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwawekea na kuwarahisishia Wajasiriamali mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zao za kiuchumi.
Mwenezi Makonda amemuahidi Mama huyo kufikisha salamu hizo za Shukrani kwa Rais Samia ,Pia alimuwezesha kiasi cha fedha ilikusudi kuongezea kwenye mtaji wa biashara yake.
Hakika huu ni upendo wa dhati wa Chama Cha Mapinduzi kwa kuwathamini, kuwajali na kuwatumikia Watanzania wote.