Katibu wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayotokana na CCM na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haimlipishi fedha mtu yeyote kuchuku mwili wa mgonjwa wao aliyefariki kutoka katika hospitalini.
Makonda amebainisha hilo alipomtaka Waziri wa Afya Ndugu. Ummy Mwalimu kueleza mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa wale ambO wagonjwa wao wamefariki na hawana hela ya kulipia maiti kwenda kuwastili ndugu zao.
Waziri Ummy akizungumza mbele ya maelfu ya Wananchi wa Tanga mjini waliojitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mwenezi Makonda, amesema kuwa Serikali chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imepiga marufuku kwa hospitali zote za Serikali kuzuia maiti ya Mtanzania yeyote na badala yake Maiti zitatolewa pasipo gharama zozote.
Aidha, Mwenezi Makonda alimtaka Waziri Ummy kutoa kauli yake kwa Watendaji wasiozingatia miongozo na maadili ambapo Waziri Ummy alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya haitamfumbia macho mtendaji ama muuguzi yeyote katika sekta ya Afya ambaye hatazingatia taratibu na miongozo ya Serikali katika kutekeleza majukumu yao na inapobainika hivyo hatua kali hasa za kuwafuta kazini zinachukuliwa dhidi yao.