Zaidi ya watu 13,000 wameuawa na wengine 26,000 kujeruhiwa katika vita vinavyoendelea nchini Sudan tangu mwaka jana, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu imetangaza Jumapili.
Sudan ilikumbwa na vita kati ya Jeshi la Kitaifa, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa Baraza tawala la nchi hiyo, na kundi la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) tangu Aprili 2023.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilisema katika taarifa yake kwamba, “Takriban watu milioni 7.6 wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan tangu mapigano yazuke.”
Kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya visa 9,700 vinavyoshukiwa kuwa kipindupindu, vikiwemo vifo 269 vinavyohusishwa, viliripotiwa nchini Sudan kufikia Januari 16.
Kamanda wa Vikosi vya Radiamali ya Haraka vya Sudan (RSF) Jenerali Mohammad Hamdan Dagalo (Hemedti) anasisitiza kuwa njia bora ya kuhitimisha mapigano nchini humo ni kuviunganisha vikosi hivyo na Jeshi la Sudan.