Shule ya Msingi ya serikali ya Michael Urio iliyopo katika kata ya Kunduchi wilaya ya kinondoni imelazimika kufungwa kwa muda baada ya maeneo ya shule hiyo kukumbwa na mafuriko ya maji yaliyotokana na mvua zilizonyesha kwa siku tatu mkoa wa Dar es salaam.
Zaidi ya wanafunzi 900 wa shule ya msingi Michael Urio uliyopo Kunduchi jijini Dar es salaam wamelazimika kutoendelea na masomo kutokana na shule hiyo kujaa maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha
Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa kata ya Kunduchi Michael Urio amesema mpaka sasa wamelazimika kufunga shule hiyo ya Watoto ya mchepuo wa kiingereza kutoendelea na masomo kwa wanafunzi kwa sababu za kiusalama ambapo ameiomba TANROADS kusaidia kujenga mitaro itakayosaidia kutoa maji katika maeneo hayo.
Shule ya Msingi Michael Michael Urio ina wanafaunzi zaidi ya mia nane ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanafunzi 500 wameandikishwa ambapo zaidi ya wanafunzi 900 watakosa kwa kuwa shule hiyo itafungwa mpaka mazingira yatakapokuwa Salama