Rais wa Namibia Hage Gaingob ataanza matibabu ya saratani baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu wa kawaida na uchunguzi wa kibaolojia uliopelekea kugunduliwa kwa chembechembe za saratani, ofisi yake ilisema.
Ofisi ya Rais wa Namibia ilisema Ijumaa kuwa mzee huyo mwenye umri wa miaka 82 alifanyiwa uchunguzi wa koloni na gastroscopy mnamo Januari 8, na kufuatiwa na uchunguzi wa kiafya.
“Kwa ushauri wa timu ya matibabu, Rais Geingob atafanya matibabu yanayofaa ili kukabiliana na seli za saratani,” ofisi yake iliongeza.
Geingob, ambaye amekuwa rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika tangu 2015, anatazamiwa kuendelea kutekeleza majukumu ya urais, pamoja na Baraza la Mawaziri, ambalo yeye ndiye Mwenyekiti.
Mnamo Juni 2023, alifanyiwa upasuaji wa aorta. Alifichua mwaka wa 2014 alipokuwa bado Waziri Mkuu kwamba alinusurika kutokana na saratani ya tezi dume.
Uchaguzi wa Rais na Bunge umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.