Mashindano ya Mpira wa miguu kwa Shule nane (8) Za msingi zilizoathiriwa na Mafuriko Wilayani Hanang Mkoani Manyara yamemalizika huku yakifanikiwa kuibua vipaji vya Soka na kujenga umoja na mshikamano.
Abdulmajid Faraj ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Save The Children akizungumza Mara baada ya kumalizika kwa Mashindano hayo alisema lengo la Mashindano hayo ni kuwarejesha wanafunzi hao katika hali zao za kawaida baada ya janga la maporomoko ya duongo kutoka katika Mlima Hanang lililotokea 3.12.23.
“Wakati Shule zimefunguliwa tuliona Mahudhurio yamekuwa madogo na tukaona tutumie huu mwanya wa Michezo kama Chachu Ya kuboresha yale mahudhurio ya watoto shuleni, lakini wakati huo huo tuweze pia kutumia michezo kama njia bora ya kuponesha yale majeraha ya kisaikolojia ya Afya ya Akili” alisema Abdulmajid Faraj ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Save The Children
Baadhi ya Wanafunzi walioshiriki katika michezo hiyo walisema imewasaidia kuamsha Ari ya kujifunza na kuwarejesha katika hali ya Kawaida licha ya athari za kisaikolojia walizozipata.