Timu ya Taifa ya Nigeria imefanikiwa kwenda hatua ya 16 Bora ya mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Guinea-Bissau katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana uliopigwa katika dimba la Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan nchini Ivory Coast.
Bao pekee la Súper Eagle alijifunga beki wa ya Ligue2 Ufaransa, Opa Sanganté dakika ya 36.
Mechi nyingine ya Kundi A wenyeji Ivory Coast walitupwa nje baada ya kutandikwa mabao 4-0 na Equatorial Guinea Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidja.
Mabao ya Equatorial Guinea yalifungwa na nyota wanaocheza timu za madaraja ya chini Hispania, mshambuliaji Emilio Nsue wa Intercity mawili dakika ya 42 na 75, viungo, Pablo Ganet wa Alcoyano dakika ya 73 na Jannick Buyla wa SD Logroñés dakika ya 88.