Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya mikopo ya IKUPA FINANCIAL SERVICE, Ikupa Steven amewatoa hofu Wananchi na Wakazi wa Kitongoji cha Kasanga na Mbuyuni katika kata ya Turiani, Mkoani Morogoro atazidi kutoa mikopo kwa wakulima ambao wanakutana na changamoto mbalimbali katika mahitaji maalumu wakati wa kuanza kilimo.
Hayo ameyasema wakati hafla fupi ya kushiriki chakula cha pamoja Wananchi na Wakazi wa kitongoji cha Kasanga na Mbuyuni kwa kuukaribisha mwaka 2024 sambamba na kutoa msaada wa mahitaji maalum kwa wenye uhitaji zaidi ikiwemo nguo, viatu na vingine vingi.
“Sisi Ikupa tunatoa mikopo kwa watu tofauti tofauti lakini lengo kubwa ni kuzidi kumsaidia mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazozifanya hasa katika kuwawezesha na kutoa mikopo kwa wenye uhitaji, mikopo yetu ni nafuu na kuna vigezo ambavyo viweza kufatwa na yeyote mwenye uhitaji zaidi” Amesema Ikupa.