Waziri wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amesema kuna athari zimeanza kujitokeza na kuhofia athari hizo kuteteresha Sekta ya Utali ya Zanzibar kufuatia Mamuuzi yaliotolewa na Bodi ya Vileo Zanzibar kwa kuwabadilisha mawakala na kupelekea Hoteli nyingi kukosa Baadhi ya Vinywaji.
Waziri wa Utali ameyasema hayo Wakati alipofanya kikao cha ghafla na Dharura na wadau hao muhimu kwenye sekta mama ya Utalii kufuatia malalamiko yaliokua yakitolewa na Wadau wa Migahawa na hoteli za Kitalii kwa Uhaba wa Vinywaji kwa Watalii
” Masikitiko yamekua ni Makubwa na imenibidi niitishe kikao kwa sababu nimeanza kuonyeshewa mkono na wadau ,mimi kama baba wa Mahoteli na Migahawa lazima nionane nao ,Sekta ya Utalii si vyema Ikachezewa chezewa tumeona Maamuzi ya Bodi ya Vileo Zanzibar imewaondosha wale waliokua wanahusika kama ZMMI,Scoch ,One Stop, nimeanza kuona athari hoteli nyingi wameanza kukosa huduma ya Vinywaji Baada ya Bodi ya Vileo kufanya Maamuzi ya Kuwaondosha wale mawakala niwaombe wawekezaji waendelee kua Wavumilivu –Waziri wa Utalii Zanzibar Simai Mohammed ”