Katibu wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi taifa, itikadi, uenezi na mafunzo, Paul Makonda ameahidi kutoa mapendekezo kwa serikali namna bora ya uwashughulikia maafisa miradi wa mikoa yote ambao hawaja kamilisha miradi kwa wakati kusimamishiwa mshahara mpaka miradi waliopewa kukamilika..
Mwenezi makonda ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake katika kijiji cha Laela wilaya ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa baada ya mradi wa hospitali kutokamilika kwa wakati na wananchi kupewa rufaa kwenda hospitali ya mbeya
‘Mimi nitapendekeza na kushawishi mbele ya safari wakubwa wanikubalie kwamba tukienda kwenye mkoa wowowte na afisa mradi ahajakamilisha mradi badsi asimamishiwe mshahara hadi atakapo kamilisha mradi kwasababu atakuwa analipwa bure hii inaonesha kuwa kuna watu hawafanyi majukumu yao ‘.
‘wagojwa wapo ndio na mashine zipo na wataalamu wapo ,serikali imenunua ila hawa viongozi wakikaa kwa viongozi wanasema tumesambaza mashine nchi nzima sasa hivi watu wanapata huduma nchi nzima lakini hawafatilii huku wagonjwa wanalipa gharama kubwa na hawafatilii bali wana kaa wakipipongezana’
‘Wengine wamepewa wizara lakini kutwa wanahangahika kutengeneza mitandao yao na vyeo na kuwalipa watu kuwasifia na wakati kwenye mamlaka na kwa watendaji wao mambo hayaendi