Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Makonda amewataka watendaji wa Mkoa wa Rukwa kuwa na utamaduni wa kusikiliza kero za wananchi badala ya kusubiri watendaji wa serikali kuu kufika kwenye maeneo yao.
Mwenezi Makonda ametoa wito huo mapema leo alipopita kwenye ukumbi wa Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga ili kuona utekelezaji wa agizo lake la Mkoa wa Rukwa kuitenga siku ya leo ili kusikiliza kero za wananchi.
Akizungumza na wananchi na wakuu wa idara mbalimbali za mkoa wa Rukwa, Makonda amehimiza pia suala la upendo na kujali ili kuhakikisha kila mmoja anaridhika na maamuzi mbalimbali yanayochukuliwa na viongozi wa Serikali.