Hifadhi ya Taifa ya Mikumi imevunja rekodi ya kupokea Watalii ambapo Kwa kipindi Cha miezi sita kuanzia mwezi julai 2023 Hadi Januari 2024 imepokea Watalii elfu 76000 huku ikitarajia kupokea Watalii 123000 Hadi kufika mwezi julai 2024
Hayo yamesemwa na Mhifadhi mkuu kitengo Cha utalii Hifadhi ya Taifa Mikumi Herman Mtei ambapo amesema filamu ya The Royal Tour inekua chachu kubwa katika kuhamasisha utalii.
Hifadhi hiyo ya Mikumi ipo Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro ambapo kutokan. Na kuwepo kwa miundombinu bora ya usafiri,Reli ya kati,uwanja wa ndege katika hifadhi hiyo na barabara kuu ya TAZAM (Morogoro -Iringa) kumesaidia kuwepo kwa ongezeko la watalii
Anasema kwa Siku hifadhi inauwezo wa kupokea Watalii 200_250 tofauti na miaka ya nyumba kabla ya ujio wa filamu ya The Royal Tour ambapo kwa sasa hamasa ni kubwa na Watalii wazawa wanazidi kuongezeka.
Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Mikumi Kamishina Agustine Masesa amesema kitendo Cha Watalii wazawa kufika katika Hifadhi ya Mikumi ni kuunga mkono jitihada za serikali kwenye sekta ya Utalii.
“ Mhe. Rais ametuonyesha njia sasa ni wakati wetu sisi watanzani kutelembelea hifadhi zetu Rais anatoka ikulu kwenda mbugani wewe ni nani usije ?”
Amesema katika Hifadhi hiyo Kuna Viwanja vya michezo mbalimbali ambapo wasanii wanashauriwa kurekodi nyimbo zao na filamu badala ya kwenda kurekodi nje ya nchi.
Msisitizo kwa jamii ni kuendelea kujtokeza kwa wengi kuweza kuunga mkono wa jitihada za Rais Samia kutangza utalii wa ndani katika nchi mbalimbali.