Huwenda hii ikawa ni Good news kwa wapenzi na watumiaji wa vifaa vya Apple, tukiwa bado mwanzoni mwa mwaka 2024 Kampuni hiyo kutoka nchini Marekani imezindua kifaa kipya cha kuvaa machoni kilichopewa jina la Apple Vision Pro.
Kwa mujibu wa Apple wenyewe wanasema kifaa hiki kitakusaidia kuona au kutazama ulimwengu kwa uhalisia ikiwa ni kidigitali zaidi.
Kifaa hiki kinatumia mfumo wa 3D, na unaweza ku- ki operate kwa kutumia mkono, macho pamoja na sauti.
Kingine kizuri kwa kutumia kifaa cha Apple Vision Pro kitakuwezesha kuingia mitandaoni na kuperuzi vitu mbalimbali kwa technolojia ya kisasa zaidi.
Mbali na hayo yote gumzo lingine ni kuhusu gharama yake kwani ili uweze kukimiliki kifaa hiki unatakiwa kutoa Dollar karibu $3499, sawa na zaidi ya milioni Tsh. 8.