Duru mpya ya mazungumzo yenye lengo la kupata “utulivu” huko Gaza na mazungumzo ya wafungwa yanatarajiwa kufunguliwa mjini Cairo, shirika la habari la AFP linaripoti.
Misri inazitaka “pande zote mbili kuonyesha kubadilika kwa lazima” kufanya makubaliano, afisa mmoja wa Misri ambaye hakutajwa jina amenukuliwa akisema.
Chanzo cha Hamas chenye ufahamu wa suala hilo kilithibitisha mazungumzo ya Cairo kwa lengo la “kusitisha mapigano, kukomesha vita, na makubaliano ya kubadilishana wafungwa”.
Haijulikani iwapo maafisa wowote wa Israel watahudhuria mkutano huo baada ya Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu kukejeli “matakwa ya ajabu” ya Hamas siku ya Jumatano.