Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim Majaliwa amesema kwasasa serikali imeruhusu wafanyabiashara wa sukari na wenye viwanda kuingiza sukari kutoka nje ya nchi ili kupunguza makali ya upatikanaji wa sukari kutokana na viwanda kusimama baada ya mashamba kujaa maji
Kauli ya WazIru mkuu Kassim Majaliwa ameitoa bungeni wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mhandisi Stella Martin Manyanya mbunge wa Jimbo la Nyasa aliyetaka kujua hali ya upatikanaji wa sukari nchini hasa kuelekea kipindi cha Mwezi wa Ramadan na Kwaresima
“Ni kweli tunaupungufu wa Sukari nchini na upungufu huu unatokana na kuwepo kwa mvua nyingi ambazo maeneo yetu ya mashamba ya miwa inayozalisha sukari maji yamejaa kiasi cha kwamba wale wamiliki wa mashamba hawawezi kutoa miwa kutoka mashambani kwenda viwandani na kweli viwanda vimebaki havina sukari,wizara imetoa vibari kwa wafanyabiashara wa sukari ikiwemo wazalishaji wenyewe kuingiza sukari nchini Zaidi ya tani laki moja na taarifa nilizonazo kutoka wizara ya kilimo tayari tumeanza kupata sukari kutoka nje na hii itaendelea kupunguza makali ya kukosekana kwa sukari nchini” Kassim Majaliwa
TAZAMA PIA.:GRISELDA BLANCO MWANAMKE HATARI ALIEISUMBUA MAREKANI, ALIMNYIMA USINGIZI PABLO ESCOBAR