Klabu ya Yanga kwa kushirikiana na Benki ya NMB wamezindua kadi mpya ya NMB Yanga World Debit Card (Black Card) ambayo sasa inampa fursa Mwanachama/Shabiki wa Yanga kupata faida mbalimbali kwa kuwa na kadi hiyo.
Kadi hiyo inapatikana kwa Tsh milioni 1 kwa mwaka, na Mwanachama au Shabiki atakayekuwa na kadi hiyo atapata tiketi 10 za VIP za mechi za nyumbani za Yanga katika msimu, jezi mpya seti sita za msimu husika, punguzo la 10% ukifanya malipo kwa kutumia kadi na utakaa VIP Lounge katika viwanja mbalimbali vya ndege duniani.
Ukikata tiketi ya ndege kwa kutumia kadi hiyo utapata na Bima ambayo mzigo wako ukipotea utalipwa hadi USD 3000.