Kiungo wa kati wa Liverpool Thiago Alcantara huenda amecheza mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo baada ya kupata jeraha jipya aliporejea dhidi ya Arsenal siku ya Jumapili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ndani ya miezi 10 alipocheza chini ya dakika ya 85 katika kipigo cha 3-1 cha The Reds huko Emirates.
Hakuna muda uliowekwa kwenye jeraha lake la hivi punde.
Thiago mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na inaonekana kwamba huenda Liverpool itampa mkataba mpya kwani majeraha yamekuwa yakisumbua muda wake huko Anfield.
Liverpool watawakaribisha Burnley Jumamosi katika mechi ya Ligi ya Premia, saa 3 usiku.