Takriban maajenti watano wenye silaha wa kundi la kulinda mazingira ambalo katika miaka ya hivi karibuni limebadilika na kuwa kundi la wanamgambo waliuawa baada ya majibizano ya risasi na polisi wa kitaifa katika mji mkuu wa Haiti, Jumatano (Feb 7), kulingana na ripoti za vyombo vya habari zilizowanukuu polisi.
Haya yanajiri huku maandamano makali ya kutaka kuondolewa madarakani kwa Waziri Mkuu Ariel Henry yameifanya nchi hiyo kuyumba.
Haiti imeshuhudia wimbi jipya la ghasia tangu Jumatatu (Feb 5) huku maelfu ya raia wa Haiti wakiingia mitaani kupinga serikali ambayo haikuchaguliwa ya Waziri Mkuu aliye madarakani na kumtaka ajiuzulu.
Haiti ilishuhudia makabiliano kati ya magenge hasimu, polisi na makundi ya kiraia ya kulinda usalama na kusababisha athari mbaya kwa wakazi wa eneo hilo ambao mara nyingi wanakabiliwa na mauaji ya kiholela, unyanyasaji wa kingono uliokithiri, uporaji, utekaji nyara kwa ajili ya fidia na uchomaji moto.
Baadaye polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliochoma matairi ya magari.
Katika taarifa yake ya kwanza tangu maandamano ya ghasia kuzuka Jumatatu, Waziri Mkuu wa Haiti ahimiza utulivu Henry katika hotuba fupi ya umma mapema Alhamisi (Feb 8).
“Nadhani wakati umefika kwa wote kuweka vichwa vyetu pamoja ili kuokoa Haiti, kufanya mambo kwa njia nyingine katika nchi yetu,” alisema.
Waziri Mkuu aliyeko madarakani pia aliwataka raia wa Haiti wasiiangalie serikali au polisi wa taifa hilo kama wapinzani wao, akiongeza kuwa wale wanaochagua vurugu kuchukua mamlaka “hawafanyi kazi kwa maslahi ya watu wa Haiti.”