Wanandoa kutokea nchini Kenya katika Kaunti ya Isiolo mnamo Alhamisi walisimulia jinsi walivyokaribia kupoteza maisha kwenye taya za simba aliyewashambulia.
Ingawa shambulio hilo la kinyama liliwaacha wakiuguza majeraha mabaya, Michael Apaiyu na mkewe Susan Chebet walisema walikuwa na bahati kuwa hai.
Alipomwona simba huyo akimfuata mkewe ambaye alikuwa akitafuta kuni katika eneo la Maili Nane, Apaiyu alikuwa na chaguo la kukimbilia kuokoa maisha yake mpendwa na kukabiliana na paka huyo mkubwa.
kulingana na The EastAfrican Apaiyu alichagua kukabiliana na simba huyo, akijua vyema hatari kubwa aliyokuwa akijianika nayo.