Mahakama ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma imemuhukumu Ruben Gerishon(24),Dereva pikipiki,mkazi wa Kijiji cha Mlela kwenda jela miaka 30 na kutaifisha pikipiki yake yenye namba za usajili MC 601 DLB aina Kinglion kuwa mali ya Serikali baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 24.
Mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 07,2023 akiwa njiani baada ya kukodiwa na muhanga kumtoa katika kijiji cha Kidahwe na kumpeleka kijiji cha Mlela katika Wilaya hiyo.
Mshitakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Septemba 11,2023.
Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Uvinza Misana Majura amesema mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na ndipo ilipomtia hatiani mtuhumiwa sawasawa na sheria.
Mshitakiwa amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria,maadili na ukatili dhidi ya wanawake.