Serikali kupitia wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iko mbioni kutengeneza sera,sheria na kanuni za kuwalinda watanzania kukabuliana na ukuaji wa teknolojia hasa ya akili bandia inayotajwa kuwa ni tishio la ajira kwa wasomi nchini
Hayo yamesemwa na Nape Nnauye Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati akijibu swali ya mbunge wa Jimbo la Kawe mchungaji Dkt. Josephat Gwajima aliyehoji ukuaji mapokezi ya matumizi ya akili bandia na matumizi ya roboti yanavyoweza kuwaondolea ajira watu wengine
“maendeleo ya sayansi na teknolojia na ubunifu duniani yametupitisha kwenye mapinduzi kadhaa ndio maana tuna mapinduzi ya kwanza ya viwanda mapinduzi ya pili mapinduzi ya tatuna sasa tupo mapinduzi ya nne na sasa kuna nchi zipo mapinduzi ya tano na ya sita kila mapindizi yaliptokea yalikua na sifa zake ,kumeku na faida na hasara ya kila mapinduzi,yakovambayo yameleta faida lakini yameleta hasara ,mapinduzi ya kwanza kuna watu walipoteza kazi na kuna watu walipata kazi” Nape Nnauye waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari