Mkuu mpya wa majeshi ya Ukraine, Oleksander Syrsky, amesema kuwa vikosi vyake vitahitaji kubadilika na kuwa tayari kubadili namna vinavyopambana na vikosi vya Urusi ili kushinda vita.
Kuteuliwa wiki hii kwa Syrsky mwenye umri wa miaka 59, ndiyo yalikuwa mabadiliko makubwa zaidi katika uongozi wa jeshi la Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi karibu miaka miwili iliyopita.
Syrsky amechukua nafasi hiyo kutoka kwa kamanda mashuhuri Valey Zaluzhny, ambaye Rais Volodymyr Zelensky amemtunuku hadhi ya Shujaa wa Ukraine.
Hata hivyo, msemaji wa ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov, amesema kuteuliwa kwa Syrsky hakutaleta mabadiliko yoyote katika mzozo huo, na kwamba Urusi itaendelea na kampeni yake ya kijeshi hadi malengo yake yatimie.