Kaimu Mhifadhi mkuu Hifadhi ya Taifa Saadani Afisa uhifadhi Simon Aweda amesema katika Hifadhi hiyo watalii wengi wamekua wakimiminika ni kutokana na kuwa na kivutio cha kipekee Nyika kukutana na bahari .
Amesema kwa afrika mashariki hiyo ndiyo Hifadhi pekee yenye kivutio hicho ambapo wageni wanapata fursa ya kuona maji ya mto yakikutana na Maji ya bahari kisha maji ya mto kutengwa pembeni.
Anasema pamoja na hayo pia wageni wanapata fursa ya kuwasogelea karibu zaidi wanyama majini ikiwemo Kiboko na Mamba Kwa kitumia usafiri wa boti tofauti na sehemu zingine wanawaona kwa mbali.
Kwa upande wake Afisa Uhifadhi Mkuu TANAPA kitengo cha Mawasiliano Catherine Mbena amesema katika kueleka Sikukuu ya wapendanao Wananchi wanakaribishwa kujumuika katika hifadhi hiyo kwa kufanya matukio mbalimbali ikiwemo ndoa,harusi ,Siku ya kuzaliwa ambapo watapata Fursa ya kufanyia katika boti wakiwa kwenye maji.
“NIwakaribishe Sana katika Hifadhi hii kumuunga mkono Rais Samia kutembelea Vivutio vingii ikiwemo Wanyama wa nchi kavu na wanyama wa majini ”