Yanga SC kwa kushirikiana na GSM Foundation ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 89 ya Klabu yao leo wamerudisha kwa jamii.
Yanga baada ya kumaliza Jogging walitembelea na kufanya usafi pamoja na kugawa msaada katika wodi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (Meta Hospital).