Watalii kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kushanganzwa na aina ya vivutio vilivyopo majini katika Hifadhi ya Taifa Saadan kwenye fukwe za Bahari ya Hindi.
Hifadhi ya Saadan imegawanyika katika maeneo mawili Nchi kavu asilimia 30 na majini asilimia 70 jambo ambalo linachangia kuvutia Watalii kutokana na aina mbalimbali za Viumbe hai vilivyopo.
Uwepo wa aina tofauti za Viumbe maji ikiwemo kamba mti na miamba ya kipekee ya mazalia ya samaki katika kisiwa cha Mafui San Bank kinachopatikana katikati ya bahari ya Hindi kumeendelea kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali na kuifanya hifadhi hiyo kuendelea kuwa maarufu duniani.
Hayo yameelezwa na Hamis Mwinyikombo ambaye ni Mwongoza watalii Hifadhi ya Saadan amesema silimia 70 katika hifadhii ya sadani ni eneo la nchi kavu na asilimia 30 ikiwa ni eneo la bahari ya hindi na kusisitiza kuwa uwepo wa Vivutio tofauti tofauti vya kitalii katika hifadhi ya saadan.
Pia amesema katika hifadhi ya saadan miongoni wa Vivutio vya kipekee ni uwepo wa kisiwa cha Mafui San Benk ambacho Watalii wengi ufika na kwenda kukiangalia ambapo maji yake ufika nchi kavu nakuacha mchanga unaovutia katika kisiwa hicho.
Kutokana na umuhimu wa hifadhi hiyo ya Saadan Afisa Uhifadhi Mwandamizi katila Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Eliasia amesema mikakati mbalimbali ya kuendelea kupokea wageni wengi zaidi inaendelea kuwekwa katika kipindi hiki cha Mwezi wa wapendanao ambapo amesisitiza watanzania kutembelea Hifadhi hiyo na ili kujionea Vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo.