Jeshi la Israel lilisema Jumapili (Feb. 11) kwamba kumekuwa na mapigano katika mji wa kusini wa Gaza wa Khan Younis katika wiki za hivi karibuni na “limewaangamiza takriban magaidi 100”.
Picha zilizotolewa na Jeshi la Ulinzi la Israel zinaonyesha wanajeshi wakiingia majumbani au wakiwa wamepanda vifaru.
Wakati wa kampeni yake ya miezi 4, jeshi la Israel limeharibu shule, hospitali, makaburi, misikiti, makanisa pamoja na maeneo ya kiakiolojia na kuacha maeneo adimu yakiwa yamebakia, haswa kaskazini mwa Gaza.
Wapalestina 27,000 wameuawa hadi sasa.
Mapigano makali bado yanaendelea katikati mwa Gaza na huko Khan Younis.
Waziri Mkuu Benyahim Netanyahu ameashiria mipango ya kusukuma operesheni ya kijeshi kusini zaidi hadi Rafah.
Operesheni ya ardhini katika eneo lenye watu wengi inaweza kukata njia moja pekee ya kuwasilisha vifaa vya kuokoa maisha kwa mamilioni ya raia waliokwama huko.