Majimbo tisa yalikumbwa na mafuriko, watu 525,000 waliathiriwa mafuriko hayo na 27 walifariki: hii ndio ripoti rasmi ya mafuriko ya mwezi Januari huko Kongo-Brazzaville. Mamlaka inaonya juu ya athari za kiafya.
Wakati mafuriko bado yanaendelea katika baadhi ya maeneo, mamlaka inatahadharisha kuhusu madhara ya kiafya yanayoweza kutokea, hasa hatari ya mlipuko wa kipindupindu. Hakuna wagonjwa walioogunduliwa kufikia sasa.
Daktari Jean-Médard Kankou, mkurugenzi wa magonjwa na udhibiti wa magonjwa katika Wizara ya Afya, anatoa wito kwa watu kuwa waangalifu:
“Kulipotokea mafuriko, kulikuwa na vyanzo kadhaa vya maji ambavyo vilichafuliwa. Kulikuwa na vijiji vizima vilivyokumbwa na mafuriko, vyoo, kila kitu kilikuwa kimejaa maji.
Na kwa hivyo, baada ya mafuriko kupungua, lazima tuogope hatari ya magonjwa yanayoibuka na magonjwa yenye uwezekano wa mlipuko kama vile kipindupindu.