Mikel Arteta amekiri kwamba Arsenal itamkosa Jorginho iwapo ataondoka msimu huu wa joto.
Kiungo huyo wa kati wa Italia aliwasili Emirates akitokea Chelsea Januari 2023 lakini amekuwa ndani na nje ya timu.
Kiungo huyo mkongwe ameonyesha kung’aa, haswa dhidi ya Liverpool mapema mwezi huu. Hata hivyo, mkataba wake na The Gunners unamalizika majira ya joto, lakini hajapewa mkataba mpya.
Akizungumza kabla ya mchezo wa Jumapili, Arteta alisema kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 bado ni mchezaji muhimu katika kikosi chake.
“Sishangai kwa sababu amefanya hivyo. Ukiangalia kazi yake na uwezo wake wa kutoKa katika mechi kubwa ni mkubwa, na ni wa ajabu. Ndiyo maana tuliamua kumleta.