Miaka kadhaa ya ghasia na ukosefu wa usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaohusishwa na makundi ya waasi umewafurusha watu milioni 5.7 kutoka makwao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu OCHA.
Hivi sasa Afrika Kusini imeamua kutuma karibu wanajeshi 3,000 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupambana na makundi ya waasi wenye silaha, ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilisema.
“Katika kutekeleza wajibu wa kimataifa wa Afrika Kusini kwa ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rais Cyril Ramaphosa aliagiza kuajiri askari 2900 wa Jeshi la Ulinzi la Taifa la Afrika Kusini kusaidia katika mapambano dhidi ya makundi haramu yenye silaha Mashariki mwa DRC,” ofisi ilisema katika taarifa.
Wanajeshi hao watatumwa DRC hadi Desemba 15, 2024, taarifa hiyo iliongeza.