Mwanariadha wa Kenya Sarah Chepchirchir amepigwa marufuku ya miaka minane baada ya mshindi huyo wa zamani wa Tokyo Marathon kugundulika kukiuka kanuni za kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa mara ya pili, kitengo cha Uadilifu cha Riadha (AIU) kilisema katika taarifa yake Jumanne.
Chepchirchir alikuwa amerudisha matokeo mabaya ya uchambuzi ya testosterone, AIU ilisema. Sampuli hiyo ilikusanywa katika mbio za Bangsaen42 Chonburi Marathon nchini Thailand mnamo Novemba.
Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 39 hapo awali alipigwa marufuku kwa miaka minne mnamo 2019, iliyorejeshwa hadi Aprili 11, 2018, kwa sababu ya ukiukwaji wa pasipoti yake ya vipimo vya damu .
Mwaka jana, AIU na Shirika la Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini Kenya walisema “operesheni iliyobobea kimatibabu” ilikuwa ikiwasaidia wanariadha wa Kenya kuficha makosa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli.