Hospitali kuu ya London imeomba msamaha kwa zaidi ya wanawake 100 baada ya mayai na viinitete vyao pengine kuharibiwa wakati wa kugandisha kwenye kliniki yake inayoendeshwa na NHS.
Kliniki hiyo, iliyopo katika Hospitali ya Guy’s mjini London Uingereza, imesema huenda ilitumia bila kukusudia baadhi ya chupa zenye hitilafu za kugandisha mayai hayo na viini tete mnamo Septemba na Oktoba 2022.
Hata hivyo, zahanati hiyo ilisema haikujua kifaa hicho kilikuwa na kasoro wakati huo.
Msemaji wa Guy’s na St Thomas ‘NHS foundation trust alisema suala la utengenezaji linaweza kuathiri vibaya uwezekano wa yai lililogandishwa au kiinitete kuishi wakati wa kuyeyuka.
Msemaji huyo alisema: “Tulifahamishwa kuhusu suala la utengenezaji wa chupa za suluhisho ambazo zinaweza kutumika kugandisha mayai na viinitete katika kitengo chetu cha utungaji mnamo Septemba na Oktoba 2022.”
Inaaminika kuwa wagonjwa wengi kati ya 136 walioathiriwa wamepata matibabu ya saratani tangu mayai au viini vyao vigandishwe, jambo ambalo linaweza kuwafanya wagumba.