Wanafunzi 1500 katika Shule ya Msingi Ludeba Iliyopo katika Kijiji cha Ludeba Kata ya Ipalamasa Halamashauri ya wilaya ya Chato Mkoani Geita wanakabiliwa na Changamoto ya uwepo wa vyoo vya Kisasa kwa wanafunzi pamoja na walimu katika Shule hiyo .
Akizungumzia Changamoto hiyo Daud Ludeba ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ludeba, amesema Shule hiyo inakabiliwa na Changamoto ya kutokuwepo hata kwa tundu Moja la Choo ambapo wanafunzi wamekuwa wakijisaidia katika Choo cha Nyasi pamoja na wanafunzi wa kike kuwa watoro kwa Asilimia kubwa.
“Baadhi ya Changamoto hizo ni upande wa Matundu ya Vyoo shule ya Msingi Ludeba ina wanafunzi 1500 na haina hata tundu Moja la Choo watoto wa kike wanashindwa kupata huduma kwa urahisi kwa asilimia kubwa ni watoro na ukiangalia Mazingira waliyopo si Mazuri, ” Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ludeba.
Aidha Mwalimu Daud William amesema Shule hiyo ina walimu 13 wanaokabiliwa na changamoto ya Nyumba za Kuishi ambapo wamekuwa wakiishi 5KM kutoka Shuleni hiyo wanayofundisha huku akiiomba Serikali kunusuru Changamoto hiyo.
Changamoto hizo Zimeibuka Mara Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Chato ,Mhandisi Deusdedith Katwale kufanya Ziara ya kutembelea Shule hiyo iliyoko katika kata Ipalamasa ambapo akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa Njia ya Simu amesema tayari kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya kwenda kunusuru Maisha ya wanafunzi hao.