Mahakama ya Rufaa ya Paris mnamo Jumatano Februari 14 imemhukumu Nicolas Sarkozy baada ya kukata rufaa kwa kifungo cha mwaka mmoja, katika kesi ya Bygmalion kutokana na matumizi mabaya ya fedha wakati wa kampeni yake ya uchaguzi wa urais ya mwaka 2012 ambapo alishindwa. Rais wa zamani amekataa rufaa kwa mahakama ya juu zaidi ya kitaifa, amesema Wakili Desry, mwanasheria wake.
Miezi sita jela ya hukumu aliyopewa rais huyo wa zamani (2007-2012) itarekebishwa, amebainisha jaji kiongozi wa mahakama akisoma uamuzi wake, na kuongeza kuwa mahakama “imerejelea adhabu iliyoombwa katika mahakama ya mwanzo na mwendesha mashitaka “.
Mnamo mwezi Septemba 2021, mahakama ya uhalifu ya Paris ilimpata Nicolas Sarkozy na hatia ya kuvuka kwa kiasi kikubwa kikomo cha matumizi ya fedha kisheria na kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kufadhili kampeni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, mahakama iliomba hukumu hii itekelezwe moja kwa moja, nyumbani, chini ya uangalizi wa kielektroniki.