Mamia ya watu waliovalia nguo nyeusi walikusanyika katika mkesha uliopewa jina la “Dark Valentine” katika mji mkuu wa Kenya siku ya Jumatano, kupinga ongezeko la mauaji ya wanawake nchini humo.
Visa vya mauaji ya wanawake nchini Kenya vinaongezeka, huku zaidi ya kesi 16 zikiripotiwa na polisi na vyombo vya habari vya ndani tangu kuanza kwa mwaka huu.
“Hatukubaliani kabisa na mauaji ya wanawake, tunapoteza wanawake wengi sana, wasichana wengi sana. Kwa hiyo leo hii wengi wetu tumeweka mipango yetu ili tuje hapa na wanawake wenzetu, mabibi wenzetu, viongozi wenzetu wa kike kuhakikisha tunamaliza.
mauaji ya wanawake,” alisema Merlin Kawira, mwanafunzi na mwanzilishi wa kikundi cha kusaidia afya ya akili chuoni kiitwacho Africa Arts and Mental Talks.
Katika siku ya kitamaduni ya kusherehekea upendo, wanafunzi walikusanyika ili kuwakumbuka wahasiriwa wa mauaji ya wanawake kwa kuwasha mishumaa, kuimba majina ya waliouawa, na kushika maua mekundu.