Emilio Nsue, mfungaji bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast amesimamishwa kwa muda usiojulikana na shirikisho la soka la nchi yake.
Mshambulizi huyo wa Equatorial Guinea alidaiwa kuhusika katika “vipindi kadhaa vya utovu wa nidhamu” wakati wa AFCON 2023 kulingana na shirikisho la Equatoguinean (Feguifut).
Nsue, 34, alimaliza kama mfungaji bora kwenye fainali hizo, akifunga mabao matano katika mechi nne za nje huku Equatorial Guinea ikitolewa katika hatua ya 16 bora. Alikuwa Abidjan Jumapili kupokea zawadi ya kiatu cha dhahabu kufuatia ushindi wa Ivory Coast dhidi ya Nigeria kwenye mechi. mwisho.
Nsue hata hivyo sio mchezaji pekee ambaye amekabiliwa na hasira ya mamlaka ya soka nchini humo. Mchezaji mwingine Iban Salvador pia amefungiwa. Kiungo huyo wa kati wa National Thunder mwenye umri wa miaka 28 alihusika katika “tukio lisilo la kufurahisha” huko Abidjan tarehe 29 Januari – siku moja baada ya timu hiyo kuondolewa kwenye dimba kulingana na Feguifut.