Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita inatarajia kutoa chanjo ya Surua rubella kwa watoto walio chini ya Miezi 9 mpaka 59 Watoto wapatao 58,000.
Akizungumza mara Baada ya kuzindua Zoezi hilo kiwilaya lililofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Mbogwe iliyopo kata ya Masumbwe Katibu Tawala wilaya ya Mbogwe Jacob Rombo amesema zoezi hilo limeanza leo February 15 na linatarajia kukamilika Feburuary 18 Mwaka huu huku akiwahimiza wazazi kuleta watoto wao ili waweze kupata Chanjo hiyo.
Aidha Katibu Tawala , Rombo amewasisitiza wahudumu ngazi ya Afya kuhakikisha wanatoa huduma hiyo kwa Usahihi pamoja na kuzingatia lugha nzuri kwa wenye uhitaji katika kuwatia matumaini na sio kutoa kauri zisizo na tija.
“Wanamasumbwe wanatoa lugha mbaya kwa wagonjwa hebu na sisi tunatoa lugha nzuri kwa wahudumu wetu tena sisi tujitathimini si ndio tujifanyie Tathimini kabla hatujamsema si ndiyo sawa Jamani lakini kwa wahudumu na watumishi wenzangu serikali ambayo kazi yenu wajibu wenu wito wenu mliopewa na mwenyezi Mungu ni kutoa huduma ya Afya ama huduma ya kitabibu, ‘” DAS, Rombo.
Kwa Upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Mbogwe Dkt.Zakayo Sungura amewataka wazazi na walezi kuwaleta watoto wao kupata chanjo kwani ni kinga kwa Mtoto kupata Maradhi mbalimbali.
Dkt. Sungura amesema Matarajio yao ni kuchanja watoto wapatao 58,000 ambapo zoezi hilo litachukua muda wa siku nne mpaka kukamilika kwake ambapo amesema msukumo katika zoezi hilo la ufunguzi limekuwa na Jicho la tofauti kwa wazazi na walezi kuleta watoto wao.