Mahakama Kuu Kanda ya Iringa chini ya Jaji Mfawidhi Ilvin Mgeta imemuachia huru Mjane Maria Ngoda ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka 22 baada ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala.
Maria Ngoda alitiwa hatiani November 03, 2023 baada ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala na uamuzi wa kuachiwa huru umetolewa leo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Ilvin Mgeta ambaye emesema kutokana na hoja zilizowasilishwa kwa upande wa Mrufani, Maria hana hatia na yupo huru.
Jaji Mgetta amesema hoja hizo zilizowasilishwa kimsingi zilionyesha mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Mjane Maria Ngoda hayakuwa na mantiki na kushidwa kuthibitika Mahakamani hapo.
Kesi hiyo ya rufaa namba 84101 ya mwaka 2023 ilisimamiwa na jopo la Mawakili kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS Kanda ya Iringa kwa ushirikiano wa Mawakili upande wa UWT.