Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro inatarajia kuwafikia watoto elfu 74,508 kwa kuwapa chanjo ya Surua na rubella kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5
Akizungumza mara baada ya kuzindua zoezi hilo mkuu wa wilaya ya kilosa Shaka hamdu shaka amesema zoezi hilo limeanza leo Februari 15 na linatarajia kukamilika Februari 18 mwaka huu huku akiwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao ili waweze kupata Chanjo hiyo.
DC shaka amesema serikali ya awamu ya sita inaendelea kuweka mazingjra rafiki katika utoaji huduma za afya ambapo ni Lazima wazazi kitumia Fursa hiyo Ili kuwakinga watoto na ugonjwa huo ambapo hauna dawa
Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya kilosa amesema ugonjwa wa surua unasababishwa na kirusi ambacho huambukizwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mtu aliyeathirika hivyo ni vema wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo
Anasema ugonjwa huo huathiri watu wa rika zote na hauna tiba njia pekee ya kuzuia kuwapatia chanjo ya surua watoto walio chini ya miaka mitano ni muhimu mtoto akamilishe ratiba ya chanjo kama inavyotakiwa ili apate kinga kamili
Kwa upande wake mratibu wa chanjo wilayani kilosa Lakia Nyayungwa amesema Virusi vya surua huweza kuathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara kiafya ikiwa ni pamoja kutoona kuwa kiziwi na upelekea ata kifo